KIBALI

by David Kyeu

KIBALI
Pinterest

KIBALI

by David Kyeu

Published May 29, 2010
45 Pages
6 x 9 Black & White Paperback
Genre: FICTION / Action & Adventure


    Find eBook/audiobook editions or buy the paperback or hardback at:

  • Looking for Kindle/Audio editions? Browse Amazon for all formats.
    Searching for the Nook edition? Browse Barnes & Noble.
 

Book Details



Kibali ni tamthilia ya mwanamke kwa jina Kisasa ambaye yuko kwenye harakati za kujikomboa kutoka kwenye wavu wa utamaduni unaompendelea mwanamume. Ni tamthilia iliyosanwa kwa migogoro, migongano, visiki na vizingiti vinavyomkabili Kisasa katika harakati alizo nazo za kujikomboa.

Kibali ni tamthilia ya lazima kwa wapenzi wa fasihi ya Kiswahili. Tamthilia hii inashughulikia swala nyeti kuhusu namna ambavyo mwanamke mwenye elimu anahusiana na jamii pana anamotoka au anamojipata.

Kwa kuandika tamthilia hii isyowekeka chini, David Kyeu amejithibitisha kuwa miongoni mwa kizazi kipya cha waandishi wa tamthilia ya Kiswahili. Anaichezea lugha ya Kiswahili kwa njia ya kipekee katika kuyasukasuka matukio ya mjini na vijijini na kuyaweka kwa njia ya kiubunifu.

 

About the Author

David Kyeu

David W. Kyeu ni mkufunzi wa Kiswahili katika chuo kikuu cha Wisconsin-Madison nchini Marekani. Mwandishi amewahi kufundisha Kiswahili pia katika chuo kikuu cha Brown nchini Marekani. Machapisho yake mengine ni pamoja na tamthilia ya Mchumba Haramu na hadithi za watoto kama vile, Sungura na Simutamba Shuleni na Nyangumi Mchoyo.

Also by David Kyeu

Beginning Swahili Workbook and Guide